User:Hyera Gerald

From Wikimedia Commons, the free media repository
Jump to navigation Jump to search

SAID AHMED MOHAMED

Said Ahmed Mohammed alizaliwa pemba huko Zanzibar, Mnamo tarehe 12 Desemba 1947. Hakubahatika kupata malezi ya baba na mama ipasavyo kwani wazazi wake walitengana akiwa mdogo sana. Hivyo alilelewa na mama zake wakuu (mama zake wakubwa), Bi. Jokhana Bi Rukia. Alisoma shule ya msingi Wete Boys,Pemba baadaye alihamia Kiembe samaki, Unguja. Kisha akapelekwa skuli ya Darajani (shule yenye watoto wenye vipaji) Unguja baadaye akaendelea na masomo yake ya sekondari katika shule ya upili ya Gulioni ambapo zamani iliitwa “King George The VI”. Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea akiwa kidato cha pili. Baada ya kuhitimu masomo yake ya sekondari alijiunga na chuo cha ualimu cha Nkurumah TTC kilichopo mjini Zanzibar mwaka 1966, ilishindikana kujiunga na kidato cha tano na sita kwani wakati huo kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hayati Abeid Aman Karume alipiga marufuku masomo ya kidato cha tano na sita. Baada ya kuhitimu chuo alifundisha shule ya msingi Kizimbani kwa wiki mbili tu, halafu akahitajika kwenda kufundisha shule ya sekondari Utaani, kuanzia 1969 hadi 1974. Saidi Ahmed Mohamed alifundisha masomo ya biologia, hesabu, kemia na pia Kiswahili. Baadaye alibahatika kusoma katika skuli ya International Correspondence kiwango cha kidato cha tano na sita. Baada ya kujiunga na kidato cha tano na sita alipanga kujifunza masomo ya sayansi lakini palikosekana vifaa vya kufanya masomo ya utekelezaji wa kisayansi yaani (practical) na hivyo alichagua kufanya masomo ya kisanaa. Mnamo mwaka 1976 Said Ahmed Mohammed alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea shahada ya kwanza katika elimu akijikita katika kusoma Isimu na Fasihi ya Kiswahili, baada ya kufuzu katika shahada hiyo alirejea nyumbani Zanzibar na kuwa mwalimu mkuu wa shule za msingi na upili za Hamamni kwa miaka mitatu. Na baadaye alirudi Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kujisajili kusomea shahada ya uzamili yaani (MA), katika Isimu Telekezi. Alipokuwa akisoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam kipawa chake kilimvutia mwalimu kutoka Ujerumani aliyefundisha Isimu Linganishi na ya kihistoria bwana Sigmund Bruner. Hapo ndipo alipopata fursa ya kuelekea Ujerumani kufanya shahada ya uzamifu yaani PhD, alijiunga na Chuo Kikuu cha Karl Marx Leipzig Ujerumani mwisho wa mwaka 1981 na kukamilisha shahada ya uzamifu mwaka 1985 na kutunukiwa shahada ya udaktari, kipindi hicho alikuwa pamoja na familia yake. Baada ya kumaliza shahada yake ya uzamifu huko Ujerumani aliteuliwa na raisi wa Zanzibar wakati huo mzee Idris Abdul Wakil, kuwa mkurugenzi wa pili wa Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI), ambayo baadaye ilikuwa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), hivyo kurejea nyumbani Zanzibar kwa miaka miwili na baadaye akaondoka kwa sababu za kisiasa na fitina za watu ambao haku wafahamu, akaelekea Kenya mnamo mwaka 1987 na kuwa mwenyekiti wa kwanza wa idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Moi mjini Eldoret na baadaye kufundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi hadi mwaka 1990. Said Ahmed Mohammed aliondoka Kenya kutokana na matatizo aliyokumbana nayo Moi-Kenya. Tatizo kubwa ni mtoto wake ambaye alifanyiwa visa mbalimbali kama vile kutafunwa meno na mtoto wa kikenya na suluhu ya kisa hicho haikuwa sahihi kwa mujibu wake. Sababu ya kisa hicho ni utundu wa watoto pamoja na kasumba ya utaifa ambayo iliwafanya kumuona ni mgeni na kuanza kumnyanyasa. Hivyo kwa kuwa hakupenda wanawe wateseke aliamua kuacha kazi kwani ilifikia hatua watoto wake hawakutakiwa kupanda gari ya shule. Alipotoka Nairobi alielekea Japan katika Chuo Kikuu cha Osaka, idara ya lugha za kigeni na hapo ndipo alipopata uprofesa. Alipotoka Osaka ndipo akaenda Chuo Kikuu cha Bayreuth, Ujerumani na kufundisha tangia mwaka 1997 mpaka 2012. Said Ahmed Mohammed alipenda kusoma, kutunga mashairi na hadithi fupi, alipokuwa darasa la tano alitungama mashairi yaliyotumiwa na walimu katika madarasa ya juu. Kazi yake ya mwanzo ni utunzi wa shairi ambalo liliitwa “Nimfuge Ndege Gani Ili Nipate Salama” mwaka 1960. Shairi hili lilifungua mdahalo mkubwa kwa wapenzi wa fasihi na wana fasihi. Baada ya hapo alipata hamu kubwa ya kuendelea kuandika. Hivyo aliandika mashairi na kupeleka redio ya Zanzibar. Alipata hamasa zaidi kutoka kwa walimu wake ambao ni Mohamed Abdallah, na Kindi Abubakary ambao waliona kipaji chake na kumsisitiza aandike. Said Ahmed Mohammed aliwahi kushiriki mashindano yaliyoanzishwa na idara ya Kiswahili BBC. Mashndano hayo yalihusu uandishi wa hadithi fupi za Kiswahili. Mara nyingi hadithi zake zilishinda, na hadithi ya “Sadiki Ukipenda” ndiyo iliyompa umaarufu, katika hadithi hii mtunzi alionesha umakini wake katika kutunga visa bunilizi ambavyo vilielezea maisha halisi ya kila siku katika jamii. Said Ahmed Mohammed alirithi kipawa cha usanii kutoka kwa mama yake mkubwa ambaye alikuwa nyakanga. Mama huyu alikuwa bingwa wa kuimba nyimbo za unyago. Pia alikuwa mtunzi mzuri wa mashairi, na alipenda sana hadithi za fasihi simulizi. Uandishi wa Said Ahmed Mohammed zaidi ya kurithi kutoka kwa mama yake mkubwa, ulitokana pia na mafunzo ya elimu ya dini ya kiislam, aliyoipata kutoka madrassa. Said Ahmed Mohammed alivutika na kuanza kusoma riwaya, riwaya ya mwanzo kuisoma ilikuwa ni riwaya ya Kiu( 1972), ikifuatiwa na Nyota ya Rehemu (1976), zilizotungwa na Mohamed M.S. Baada ya kusoma riwaya ya Kiu ndipo alipopata hamu na shauku ya kuandika riwaya. Riwaya yake ya mwanzo aliyoiandika ni Asali Chungu (1977), ikifuatiwa na Utengano (1980), na Dunia Mti Mkavu (1980). Aliendelea na jitihada za uandishi hadi kuwa muandishi maarufu na kupata tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Vilevile amebobea katika ushairi ambapo ametunga diwani mbalimbali, zikiwemo za kisiasa, kiuchumi, mapenzi na utamaduni. Diwani hizo ni kwa lengo la kuibua maudhui aliyokusudia muandishi huyu kama waandishi wengine wa kazi za fasihi. Ametumia fani katika kazi zake za fasihi mojawapo ya mitindo aliyotumia ni uhalisia mazingaombwe katika kazi kama vile, “Babu alipofufuka, Kivuli Kinaishi, Amezidi na Sadiki Ukipenda, pia alitumia bunilizi, utomeleaji na taswira katika kazi zake nyingi. Said Ahmed Mohammed ametajwa kama muandishi mashuhuri zaidi Africa Mashariki na hata Afrika nzima akiwa ameweza kuandika Riwaya, Tamthilia na Mashairi, kazi za watoto na hata vitabu vya shule na vyuo. Baadhi ya kazi zake zimetafsiriwa kwa lugha za kigeni, pia kuna miswada ambayo imechapishwa hivi karibuni ya riwaya ya Nkama dume, Mhanga Nafsi yangu, na kitabu cha kusoma katika darasa la saba kiitwacho Gharama ya Amani kinachozungumzia fujo za kisiasa zilizotokea Kenya. Mwandishi huyu ni miongoni mwa waandishi wa riwaya za kimapinduzi na kifalsafa. Profesa Said Ahmed Mohammed ana mke mmoja anayeitwa Rahma, na watoto wawili msichana na mvulana. Msichana anaitwa Najima jina linalo maanisha nyota na wa kiume anaitwa Mahirna neno la kiarabu lenye maana ya mwenye ujuzi na wote wamekamilisha shahada ya kwanza. Profesa Said Ahmed Mohammed Ameandika zaidi ya vitabu 60, cha karibuni zaidi kikiwa Mashetani Wamerudi, tamthilia iliyozinduliwa rasmi Oktoba 10, 2016 katika Tuzo za Kumi - Kumi ambazo hutolewa kila mwaka na mwasisi wa WASTA Kituo cha Kiswahili Mufti, Guru Ustadh Wallah Bin Wallah. Baadhi ya vitabu alivyoandika ni kama ifuatavyo: Ushairi Kama vile: Sikate Tamaa (1980) Longman Kenya Ltd. Kina cha Maisha. Jicho la Ndani (2001), Nairob: Longhorn Publisher. Tamthiliya; Pungwa (1988), Longman Kenya Ltd. Kivuli kinaishi (1990), Oxford University Press. Amezidi (1995), East African Educational Publishers. KitumbuakimeingiaMchanga (2004) Nairob: Longhorn Publishers ltd Posaza Bi Kisiwa Riwaya; Asali Chungu( 1989), East Afracan Publishers. Babu Alipofufuka (2001), JomoKenyatta Foundation. Utengano (1980), Longhorn Publishers. Tata za Asumin i(1990), Longman Kenya. Dunia Mti Mkavu (1980), Longman Kenya Ltd. Kiza Katika Nuru (1988), Oxford University Press. Dunia Yao (2006), Nairob:Oxford University Press.